Good Morning mtu wangu, uchambuzi wa magazeti @CloudsFM umekupita? Ninazo zile zote kubwa kubwa za leo kwenye kurasa za magazeti, baadhi zikiwa…
Mbowe afichua mchezo chafu kati ya CCM na NEC, Dk John Magufuli atoa siri ajira za madereva, siri ya Utafiti hadharani taasisi iliyombeba Lowassa, UKAWA waonya wizi wa kura, wagombea wa ACT Wazalendo watishiwa maisha na kuna stori ya Zitto Kabwe na Kafulila kushambuliana.
Askofu msaidizi wa Jimbo la Bukoba Methodius Kilaini ametaja sifa 8 za kumtambua Rais alietoka kwa Mungu, baadhi zikiwa; mgombea Muadilifu, Mchapakazi, mgombea atakayekuwa anatekeleza jukumu lake ipasavyo, hali ya uzalendo wa kweli na pia awe muadilifu wa Mungu, Mgombea Urais kupitia CHAUMMA, Hashim Rungwe anasema ana matumaini makubwa kuingia Ikulu na kuiongoza nchi kwa awamu ya tano.
Mgombea Urais kutoka ACT Wazalendo Anna Mgwila asema Tanzania hawana sababu ya kuwa maskini ila ni kutokana na mfumo mbaya wa Serikali, Lowassa asema CCM mwaka huu itasombwa na mafuriko, hofu ya uchaguzi yatanda juu ya wafanyabiashara huku wengi wakisema wanasubiri upepo huo wa uchaguzi kupita ili kufanya biashara, Magufuli asema CCM haiwezi kung’oka madarakani kama jino, NEC imewaomba UKAWA waache kupotosha umma ili wafanye kazi yao.
Edward Lowassa asema ameamua kuwania Urais kwa sababu CCM wameshindwa kuondoa umasikini kwa miaka 50, Dk. John Magufuli asema anashangazwa na watu wanaotaka CCM kung’oka madarakani kirahisi rahisi, Zitto Kabwe na David Kafulila washambuliana kwa vita ya maneno kwenye mitandao ya kijamii wa ‘Whatsapp’ na mwili wa Celina Kombani kuagwa leo kwenye viwanja vya Karimjee.
Hapa chini ipo sauti ya uchambuzi wote wa magazeti kwenye #PowerBreakfast bonyeza plazy kusikiliza.
PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia kuanzia kwenye siasa, muziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata, pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>> YouTUBE