Nimekutana na stori moja kwenye mitandao inayohusiana na magereza ya zamani ya wafungwa, yamekusanywa magereza 9 ya sehemu mbali mbali duniani na kubadilishwa kuwa kitu tofauti kabisa, na ukiyaona hutoamini kuwa majengo hayo yalishawahi kuwa magereza ya wafungwa!
Kwenye yale maeneo ambayo Serikali waliacha kuyatumia kama maeneo ya magereza ya wafungwa yamechukuliwa na kubadilishwa kuwa hoteli au shule mtu wangu, majengo ni yale yale sema ubunifu mdogo tu umetumika kuyageuza majengo hayo kuwa sehemu ya vivutio kwa watalii.
Na kwa msaada wa teknolojia ya kisasa kabisa sehemu hizi zimegeuzwa kuwa sehemu nzuri sana, zenye mvuto na kama ukitembelea maeneo hayo bila kujua historia ya sehemu hiyo itakuwa vigumu sana kwa wewe kujua kuwa jengo au eneo hilo lilikuwa la wafungwa magereza.
Hapa chini nimekusogezea picha 9 za maeneo na magereza mbali mbali duniani ambayo kwa sasa zinaweka headlines tofauti na miongoni mwa picha hizi kuna moja kutoka Lagos Nigeria iliyoweka headlines.
PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia za siasa muziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos