Kila siku asubuhi huwa nazisogeza headlines zilizobebwa kwenye kurasa za Magazeti ya Tanzania, Uchambuzi wa stori zote napandisha kwenye account yangu ya Twitter >>>@millardayo. Tayari nimezikusanya na waweza kuzipata huko.
Moja ya taarifa zilizoandikwa kwenye magazeti ya October 25 2016 ni hii kutoka gazeti la Nipashe yenye kichwa cha habari ‘Nyimbo za Rihanna zinatuliza maumivu wakati wa upasuaji’
#NIPASHE Utafiti umeeleza kuwa kumsikilizisha mgonjwa nyimbo za Rihanna, kunamsaidia mgonjwa kupunguza maumivu wakati wa upasuaji pic.twitter.com/mIO88H44RL
— millardayo (@millardayo) October 25, 2016
Gazeti hilo limeripoti utafiti unaodai kuwa kumsikilizisha mgonjwa nyimbo za mwanamziki maarufu wa muziki ‘pop’ Rihanna, kunamsaidia mgonjwa kupunguza maumivu wakati wa upasuaji pia kunamfanya aweze kupumua vizuri bila ya msaada wa hewa ya oksijeni.
Utafiti huo ulioendeshwa na wataalam wa hospitali ya watoto ya Lurie Chicago Marekani, umeonyesha kuwa watoto waliosikiliza nyimbo za Rihanna kwa dakika 30 wakati wa upasuaji hawakuhisi maumivu na walipumua vizuri.
Jambo hilo limefanywa chini ya utafiti wenye kulenga kutibu kwa njia ya sauti (audio therapy) unaoendeshwa na jopo la madaktari wanaoongozwa na Dk. Santhanam Suresh.
Akieleza suala hili katikaa taarifa ya utafiti wa Dk. Suresh alisema ‘Audio Therapy’ inapaswa kuchukuliwa na hospitali kama njia muhimu na bora ya kuondoa maumivu kwa watoto wanaofanyiwa upasuaji mkubwa.
Utafiti huo unachukuliwa kama sehemu muhimu ya mabadiliko ya upasuaji katika hospitali nyingi duniani kwa vile tiba ya upasuaji kwa sasa hufanywa bila ya mgonjwa kupewa dawa za kupoteza fahamu zake, maarufu kama nusu kaputi.
Kabla ya utafiti huo, Wataalamu wa masuala ya saikolojia walishagundua njia ya kutuliza akili za wagonjwa kwa kutumia rangi na wameielezea rangi ya pinki kama moja ya rangi zinazotuliza akili haraka kuliko rangi nyingine.
Wanasema kupaka rangi hiyo kwenye wodi au vyumba vya kulala, kunasaidia mgonjwa na mtu wa kawaida kutuliza akili yake na kutokuwa na mawazo mengi ikilinganishwa na rangi nyingine.
Unaweza kupitia ghabari nyingine kwenye magazeti ya Tanzania
#MWANANCHI Maofisa polisi wawili wakamatwa na magari ya wizi Moshi, wakazi wahoji kutowajibishwa kwao, uongozi wasema uchunguzi unaendelea pic.twitter.com/5xOpSf70BG
— millardayo (@millardayo) October 25, 2016
#MWANANCHI Mahakama ya mafisadi mbioni kuanza huku muda wa kusikiliza na kukamilisha mashauri ukiwa usiozidi miezi tisa pic.twitter.com/KEgVHyWaFi
— millardayo (@millardayo) October 25, 2016
#MWANANCHI Tanzania na Morocco zimetiliana saini mikataba 21 ya kibiashara, ikiwamo ujenzi wa uwanja wa mpira utakaogharimu dola mil 100 pic.twitter.com/DQYNKQbFl4
— millardayo (@millardayo) October 25, 2016
#MTANZANIA Aliyekuwa Mkurugenzi wa TPA, Ephraim Mgawe ameburutwa tena mahakamani akikabiliwa na kesi mpya ya kuomba rushwa ya Sh. bil 8 pic.twitter.com/Uh3g473tXx
— millardayo (@millardayo) October 25, 2016
#MWANANCHI Mtego uliowekwa na polisi barabara ya Bagamoyo-Msata, uliwezesha kunaswa wezi pamoja na gari waliloiba la ofisa wa JWTZ, Dallu pic.twitter.com/D7jWdnb8c9
— millardayo (@millardayo) October 25, 2016
#MTANZANIA Majina hewa saba yamegundulika ktk orodha ya watu walioandikishwa kwa ajili ya kupewa msaada kwa walioathiriwa na tetemeko Bukoba pic.twitter.com/S3tkdnNUeY
— millardayo (@millardayo) October 25, 2016
#NIPASHE Vigogo watatu wa zamani wa TPA, akiwemo aliyekuwa mkurugenzi mkuu, Mgawe wafikishwa mahakamani kwa kuomba, kutoa rushwa ya bil 8.76 pic.twitter.com/rtEdUsLH7A
— millardayo (@millardayo) October 25, 2016
#NIPASHE Watanzania wanaosafiri kwenda nchi za ughaibuni kwa safari zinazohitaji viza, watalazimika kuziombea Dom muda si mrefu kutoka sasa pic.twitter.com/mvoqVp1Q1w
— millardayo (@millardayo) October 25, 2016
#NIPASHE Watu wasiofahamika wamevamia ktk kampuni inayouza magari ya Yutong ya Benbros iliyopo DSM na kupora zaidi ya mil 80 pic.twitter.com/dYAKH9a3Hj
— millardayo (@millardayo) October 25, 2016
#NIPASHE Serikali za mitaa imetajwa kuongoza kwa vitendo vya rushwa kisekta nchini, kutokana na kuwa na kesi nyingi zinazoendelea mahakamani pic.twitter.com/JN6KNfjA4I
— millardayo (@millardayo) October 25, 2016
#NIPASHE Kampuni ya vifaa vya elektroniki ya Samsung A.Mashariki kurejesha fedha kwa wateja simu za note 7 watakaodhibitisha manunuzi yake pic.twitter.com/qO5H7vn0lP
— millardayo (@millardayo) October 25, 2016
#NIPASHE Watu watano wenye ulemavu wa ngozi wamepoteza maisha mkoani Tanga kutokana na ukosefu wa losheni za kuzuia mionzi ya jua pic.twitter.com/OkjWXip0aG
— millardayo (@millardayo) October 25, 2016
#JamboLEO Jaji mkuu wa Tanzania, Mohamed Chande ameshauri mahakimu watakaoshitakiwa kwa rushwa waondolewe kazini pic.twitter.com/ejgkHDNaBx
— millardayo (@millardayo) October 25, 2016
#UHURU Mkurugenzi wa kiwanda cha kusindika Nyama Arusha aangua kilio kisa NEMC kumzungusha kupata hati ya mazingira ili kiwanda kianze kazi pic.twitter.com/yQdW3sr5m7
— millardayo (@millardayo) October 25, 2016
#TanzaniaDAIMA Bunge lakabiliwa na ukata, baadhi ya idara, ofisi zake zadaiwa kuwa na uhaba wa vitendea kazi pia wabunge washindwa kusafiri pic.twitter.com/11DC5iM8qp
— millardayo (@millardayo) October 25, 2016
#TanzaniaDAIMA PAC yagoma kujadili hesabu za PSPF kufuatia kilichoelezwa dharau iliyofanywa na katibu wizara ya fedha dhidi ya kamati hiyo pic.twitter.com/nWqinK9xnX
— millardayo (@millardayo) October 25, 2016
#TanzaniaDAIMA Uongozi UDART umesema sababu za mabasi yao kuchelewa vituoni inatokana na kusimamishwa kwa muda mrefu na askari pic.twitter.com/YvsHQNDn6l
— millardayo (@millardayo) October 25, 2016
#MTANZANIA Wakazi wa Sisimba Mbeya walalamikia mradi wa ukarabati barabara ya mita 400 ambao umedumu kwa miaka miwili sasa bila kukamilika pic.twitter.com/oCKULljwAa
— millardayo (@millardayo) October 25, 2016
ULIKOSA UCHAMBUZI WA MAGAZETI KUTOKA AYO YV OCTOBER 25 2016? UNAWEZA KUIANGALIA VIDEO HII HAPA CHINI