Taarifa ambayo imetolewa na kaimu mkurugenzi mkuu wa mawasiliano, IKULU Gerson Msigwa imesema kwamba Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amewathibitisha watendaji wakuu wa taasisi mbili za serikali.
Waliothibitishwa ni Alphayo Kidata, aliyekuwa Kaimu Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ambaye sasa ni anakuwa Kamishna Mkuu wa TRA na Valentino Mlowola aliyekuwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), ambaye sasa anakuwa Mkurugenzi Mkuu wa (TAKUKURU).
Watendaji hawa wamethibitishwa kuanzia leo tarehe 13 Machi, 2016
ULIKOSA KUMUONA HUYU MCHEKESHAJI ANAEIGILIZIA SAUTI ZA RAIS MSTAAFU KIKWETE NA RAIS MAGUFULI? TAZAMA HII VIDEO HAPA CHINI
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE