Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo April 6, 2017, amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Umoja wa Ulaya nchini Roeland Van De Geer akiushukuru Umoja huo kwa msaada wao.
Umoja wa Ulaya umetoa msaada wa Euro Milioni 205 ambazo ni sawa na Tsh. Billion 500 kwa Tanzania kuunga mkono shughuli za maendeleo kwa kipindi cha miaka minne ijayo kuanzia mwaka huu.
“Katika mpango wao wa kuisadia Tanzania, kuna Billion 1.2 ambazo zitatolewa katika mipango ya maendeleo ya nchi yetu. Na hii itasaidia pia kuimarisha katika shughuli za viwanda, energy, infrastructure pamoja na kilimo.” – Rais Magufuli.
Aidha Rais Magufuli pia amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Israel nchini Tanzania Yahel Vilan na kumhakikishia kuwa Tanzania imedhamiria kuimaisha uhusiano uliopo baina ya nchi hizo mbili.
Bonyeza play kutazama…
VIDEO: Mambo saba waliyoongea CUF ikiwemo kupinga matokeo ya EALA. Bonyeza play kutazama.