July 29 2016 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ameanza ziara ya siku nne katika mikoa ya Singida, Tabora, Shinyanga na Geita akitokea mkoani Dodoma ambapo amezungumza na wananchi kwa lengo la kuwashukuru kwa kumpigia kura katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana na kueleza juhudi zinazofanywa na serikali katika kutatua kero za wananchi na kuwaletea maendeleo.
Rais Magufuli akizungumza na wananchi wa Manyoni Singida kuhusu madai yaliyotolewa na vyama vya upinzania kuhusu kuzuia shughuli za kisiasa, Rais Magufuli amesema >>>mimi nitazungukia majimbo yangu yote nikawaeleze wananchi nitakachokifanya kwa kipindi cha miaka mitano kwa hiyo kama upo mbunge zunguka kwenye jimbo lako mpaka uchoke, ni lazima muelewe sijazuia shughuli za siasa za watu waliochaguliwa
NI KWELI RAIS MAGUFULI ANAKATAA USHAURI? MZEE MAKAMBA KAFUNGUKA KWENYE HII VIDEO HAPA CHINI