Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli amesema kuwa Serikali ilikwishatenga eneo la maziko kwa Viongozi Wakuu wa Serikali watakaofariki, ambapo watazikwa Dodoma, kwa kuwa ndiko yaliko Makao Makuu ya Nchi.
“Kuna wakati Serikali ilipanga mahali pa maziko kwa viongozi na tulipangiwa kuwa tunazikwa Dodoma, Mzee Mkapa akaniuliza mlipanga maziko yawe Dodoma, mimi msinizike Dodoma nikasema wewe unataka wakuzike wapi akasema Lupaso” Rais Magufili
Mzee Kikwete akasema Msoga, nikaogopa kumuuliza Mzee Mwinyi kwa sababu alikuwa na miaka zaidi ya 90 na mimi nilisema nitazikwa Chato” Rais Magufuli
“Mkapa alipenda kwao, kwenye hili Watanzania tujifunze, Mzee Mkapa angeweza kuzikwa DSM au Lushoto, lakini ndani ya dhamira yake alitaka azikwe mahali alipozaliwa” Rais Magufuli