Rais Magufuli leo April 11, 2017 amepokea ripoti ya utendaji kazi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa ‘TAKUKURU’ kwa mwaka 2015/2016 iliyowasilishwa na Mkurugenzi Mkuu, Kamishna Valentino Mlowola.
Taarifa hiyo imewasilishwa kwa Rais Magufuli kwa mujibu wa sheria ya TAKUKURU ikieleza juu ya mafanikio katika kuzuia na kupambana na rushwa, mfumo wa utendaji kazi wa TAKUKURU na changamoto zilizojitokeza ambapo kutokana na nia thabiti ya Serikali ya Awamu ya Tano kukabiliana na rushwa, wananchi wameitikia kwa wingi kutoa taarifa za vitendo vya rushwa na kumekuwa na ongezeko kubwa la kesi za rushwa ambazo zinafikishwa Mahakamani.
Rais Magufuli ameipongeza TAKUKURU kwa mafanikio iliyoyapata na kuahidi kuwa Serikali itaendelea kuunga mkono juhudi hizo ili kufanikisha vita dhidi ya rushwa.
“Rushwa tukiiacha iendelee tutakwama, kwa hiyo niwaombe Watanzania na vyombo vyote vinavyohusika vitoe ushirikiano mkubwa kwa TAKUKURU, lakini nitoe wito kwenu TAKUKURU, sijaona watu wakifungwa sana kwa makosa ya rushwa.” – Rais Magufuli.
Bonyeza play kutazama hapa chini…
VIDEO: Ushauri wa Nape Nnauye kwa Rais Magufuli. Bonyeza play kutazama.