Kesi ya wafanyabiashara maarufu Mohamedi Yusufali na Samuel Lema wanaotajwa kuiibiwa serikali milioni 7 kwa dakika imeendelea leo July 28 2016 mahakama ya hakimu mkazi Kisutu kwa kusikiliza hoja iliyotolewa na upande wa utetezi wakitaka kufutwa kwa shitaka la 221 la utakatishaji fedha wakidai kuwa lina mapungufu.
Kwa upande wa Jamhuri umeiambia mahakama hiyo kuwa shitaka hilo lipo sawasawa kisheria na kwasababu hiyo hakuna haja ya kufutwa kama upande wa utetezi wanavyotaka. Kesi hiyo imeahirishwa na itaendelea tena August 10 2016.
Yusufali anadaiwa kuwa kati ya January 2008 na January mwaka huu kwa vitendo viovu vya kughushi na kuwasilisha nyaraka za uongo kwa Kamishna wa Mamlaka ya Mapato nchini TRA ameisababishia serikali hasara ya Shilingi BILIONI 15.6 ambazo zilitakiwa kulipwa kama Kodi ya Ongezeko la Thamani.
ULIKOSA WALICHOKIJIBU CCM BAADA YA CHADEMA KUTAKA MAANDAMANO? UNAWEZA KUTAZAMA VIDEO HII HAPA CHINI