Mahakama ya Rufaa nchini Misri imeagiza uchunguzi wa muda mrefu wa Mashirika 20 yasiyo ya Serikali (NGOs) yanayotuhumiwa kupokea fedha kinyume ya Sheria kufungwa.
Jaji wa Mahakama hiyo, Ali Mokhtar pia ametoa amri kwa Mashirika hayo kutofunguliwa kesi, watu 43 wakiwemo raia wa Misri, Marekani, Ulaya walifunguliwa mashtaka.
Desemba waka 2011, Mamlaka nchini humo zilivamia Makao Makuu ya NGOs hizo zikiwemo Freedom House ya Marekani, International Republican Institute na National Democratic Institute.
Vyombo vya habari vya Serikali viliwashutumu kuhusika katika njama za kuvuruga utulivu wa nchi hiyo, kesi ambayo ilidhoofisha uhusiano kati ya Cairo na utawala wa Obama.