Mahakama kuu nchini Brazil itaendelea na kesi ya Italia dhidi ya nyota wa zamani wa kandanda Robinho, ambaye alihukumiwa huko Uropa kifungo cha miaka tisa kwa ubakaji.
Katika uamuzi uliotolewa Jumatano jioni, mahakama ya juu zaidi ya Brazil ilipanga tarehe 2 Agosti kuamua ikiwa serikali ya Italia lazima itafsiri kesi kamili ya Robinho kwa Kireno na kisha kuituma kwa mamlaka ya Brazil kwa uchambuzi zaidi, kama ilivyoombwa na wakili wa mchezaji huyo wa zamani.
Mamlaka ya Italia inamtaka Robinho mwenye umri wa miaka 39 kutumikia kifungo chake nchini Brazil, lakini mahakama ya Brazil bado haijakubali yaani Brazil haiwakabidhi raia.
Robinho alipatikana na hatia nchini Italia mwaka 2017 kwa sehemu yake katika kundi la unyanyasaji wa kingono mjini Milan lililofanyika miaka minne hapo awali, alipokuwa akiichezea timu ya Serie A ya AC Milan.
Mahakama kuu ya Italia iliidhinisha hukumu ya Mbrazil huyo mwaka 2022, ambapo waendesha mashtaka wa Italia walitoa hati ya kimataifa ya kukamatwa.
Mawakili wake, ambao hawakujibu ombi la maoni kutoka kwa The Associated Press, wanadai alikuwa na mahusiano ya kimapenzi ya kimakubaliano kwenye baa na mwanamke mchanga, kama marafiki zake watano pia walivyofanya.
Ikiwa mahakama ya Brazili itakataa ombi la Robinho la tafsiri kamili kutoka Italia, itaweza kutoa uamuzi kuhusu mustakabali wake.