Mahakama ya katiba nchini Senegal Alhamisi ilibatilisha uamuzi wa kuahirisha uchaguzi wa rais uliopangwa kufanyika mwezi huu, hatua ambayo iliitumbukiza nchi hiyo katika mzozo mbaya kwa miongo kadhaa.
Mahakama hiyo ilisema sheria iliyoidhinishwa na bunge tarehe 5 Februari kuahirisha uchaguzi kwa miezi 10 na kufanya Rais Macky Sall kusailia madarakani hadi mwishoni mwa muhula wake, ni kinyume cha katiba, kulingana na waraka uliochapishwa kwenye mitandao ya kijamii na kuthibitishwa na chanzo ndani ya mahakama hiyo.
Mahakama hiyo ya katiba ilibatilisha pia amri ya Sall ya tarehe 3 Februari kurekebisha ratiba ya uchaguzi wiki tatu tu kabla ya uchaguzi, na kuahirisha uchaguzi kuanzia Februari 25 hadi Disemba 15.
Hatua ya Sall ilizua malalamiko makubwa kutoka kwa upinzani na mashirika ya kiraia ya Senegal, ambayo yaliitaja kama “mapinduzi ya kikatiba”.