Mahakama ya Hakimu Mkazi katika Jimbo la Kano Kaskazini mwa Nigeria imeamuru Mwanaume mmoja aliyetambulika kwa jina la Malam Yusuf, kumchinja jogoo wake siku ya Ijumaa au kabla kwa kosa la kusababisha uchafuzi wa mazingira kupitia makelele.
Hakimu Halima Wali alitoa agizo hilo mapema wiki hii baada ya jirani yake Yusuf kumshtaki akilalamika kwamba kuwika kwa jogoo kila mara kunamnyima usingizi.
Gazeti la Vanguard la nchini Nigeria limeripoti kuwa Hakimu Mkuu alisisitiza kuwa kitendo cha ndege huyo kuendelea kufugwa inaleta kero kwenye mtaa huo hivyo kumtaka Yusufu kuhakikisha anamchinja jogoo huyo kabla ya Ijumaa kama atakavyoamriwa au atakabiliwa na adhabu kutoka kwa Mahakama.