Mahakama ya Tanzania imeanzisha kituo jumuishi kitakachoshugulikia mashauri ya mirathi, ndoa na familia, Mkoa wa Dar es Salaam, ili kuwezesha upatikanaji wa haki kwa haraka na wakati.
Naibu Msajili Mwandamizi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Messeka Cheba, ameyasema hayo, mbele ya kamati ya Bunge ya Katiba na Sheria na kuongeza kwamba, kituo hicho kilichojengwa Temeke, Dar es Salaam, kitajumuisha wadau na wadaawa wote muhimu wa kesi hizo.
Amesema katika utafiti walioufanya mwaka 2017/18, walibaini pamoja na mambo mengine, kulikuwa na mashauri zaidi ya 5,000 ya masuala ya mirathi, ndoa na familia, hivyo Mahakama ikaamua kuanzisha kituo hicho katika majengo yake sita iliyojenga kama vituo jumuishi.