Jaji mmoja wa mahakama ya serikali mjini New York, ametupilia mbali juhudi za rais wa zamani wa Marekani Donald Trump za kuondolewa mashitaka ya ubakaji yaliowasilishwa na mwandishi E, Jean Carroll, kwamba alimharibia jina kwa kupinga kwamba hakufanya hivyo katikati ya miaka ya 90.
Jaji Lewis Kaplan akiwa kwenye mahakama ya Manhattan, New York, amepinga ombi la Trump kwamba alikuwa analindwa dhidi ya mashitaka kutokana na cheo chake cha urais. Trump alidai kwamba Carroll alisubiri kwa miongo kadhaa kabla ya kuwasilisha malalamishi yake na kwa hivyo hakuwa na budi ila kujitetea.
Mawakili wa Trump wala wa Carroll hawajasema lolote kutokana na hatua hiyo. Carroll alifunguka mara ya kwanza hapo Juni 2019, pale aliposhtumu Trump kwamba alimshambulia kwenye chumba cha kujaribia mavazi kwenye duka la Bergdorf Goodman, kwenye kitongoji cha Manhattan, wakati Trump akikanusha kumfahamu na kusema kwamba Carroll hakuwa aina ya wanawake awapendao.
Carroll anaomba kulipwa ridhaa ya takriban dola milioni 10, na kesi yenyewe imepangwa kusikilizwa Januari 15 mwaka ujao.
Raisi wa zamani Donald Trump mnamo Alhamisi ya tarehe 20 machi alikemewa na jaji katika kesi yake ya ubakaji ya raia inayokaribia juu ya ombi la majaji kuambiwa kwamba ikiwa rais huyo wa zamani hatatoa ushahidi, itakuwa kwenye wasiwasi kwamba uwepo wake ungeathiri vibaya jiji la New York.
Wiki iliyofuata wakili wa Trump, Joe Tacopina, alijaribu kwanza kuchelewesha kesi kisha akaomba maagizo ya jury.
Katika barua kwa jaji wa shirikisho Lewis A Kaplan siku ya Jumatano, Tacopina alisema majaji wanapaswa kuambiwa: “Ingawa hakuna mlalamishi anayehitajika kufika katika kesi ya madai, kutokuwepo kwa mshtakiwa katika kesi hii, kwa kubuni, kunaepuka mizigo ya vifaa ambayo uwepo, kama rais wa zamani, ungesababisha mahakama na jiji la New York.
chanzo:VOA