Jenerali Mahamat Idriss Deby Itno, ambaye ameongoza serikali ya Chad kwa miaka mitatu iliyopita, ataapishwa Alhamisi baada ya ushindi wa uchaguzi unaopingwa vikali na vyama vya upinzani katika taifa hilo la Afrika ya kati.
Deby alishinda rasmi asilimia 61 ya kura za Mei 6 NGOs za kimataifa zilisema haziaminiki wala hazikuwa huru, na ambazo mpinzani wake mkuu aliziita “kinyago”.
Deby alitangazwa rais wa mpito Aprili 2021 na junta ya majenerali 15 baada ya baba yake, rais Idriss Deby Itno, kuuawa kwa kupigwa risasi na waasi baada ya miaka 30 madarakani.
Kuapishwa huko kunaashiria mwisho wa miaka mitatu ya utawala wa kijeshi katika nchi muhimu kwa mapambano dhidi ya waasi katika eneo lenye machafuko la Sahel barani Afrika.