Ikiwa ni wiki moja imepita toka klabu ya soka ya Simba imlete kiungo wa kimtaifa wa Zimbabwe aliyekuwa anacheza soka la kulipwa katika klabu ya Vicem Hai Phong F.C ya Vietnam Justice Majabvi ambae ni mara yake ya kwanza kucheza Simba na amecheza mechi yake ya kwanza ya kimataifa toka ajiunge na Simba.
Majabvi aliongea katika exclusive interview na millardayo.com namna ambavyo anajisikia furaha kuwa katika klabu ya Simba na kucheza mechi yake ya kwanza, Majabvi amekiri kuzifahamu Simba na Yanga kama klabu ya kubwa za Tanzania lakini alikuwa hafahamu kitu kingine zaidi.
“Najisikia furaha kucheza mechi yangu ya kwanza na huu ushindi ni kama booster ya kuendelea kufanya vizuri na najisikia vizuri Tanzania ni kama nipo nyumbani kwani Tanzania ni karibu na kwetu na furaha sana na ushindi huu ni kama kukaribishwa kwangu”>>>Justice Majabvi
Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 31 amewahi kuichezea timu ya Dynamos na kufikia hatua ya Nusu Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika mwaka 2008, kwa mara ya kwanza alicheza timu ya taifa ya Zimbabwe July 15 2004 dhidi ya timu ya taifa ya Zambia.
Zaidi msikilize hapa Justice Majabvi
PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia za siasa muziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos