Muonekano wa Ujenzi wa Shule mpya maalum ya Sekondari ya Bweni na sayansi ya Wasichana katika Mkoa Ruvuma kuanzia kidato cha kwanza mpaka cha sita iliyosajiliwa rasmi kwa jina la Dkt. Samia Suluhu Hassan inayojengwa katika Halmashauri ya Wilaya Namtumbo.
Ujenzi wa shule hiyo Mpya unatekelezwa kupitia Mradi wa kuboresha Elimu ya Sekondari (SEQUIP) kwa gharama ya shilingi bilioni 4 ambapo Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa ameweka jiwe la msingi la ujenzi wa shule hiyo.leo tarehe 06 Januari 2023.
Uienzi unatekelezwa kwa awamu mbili ambapo awamu ya kwanza ya utekelezi wa mradi huo ulianza tarehe 6 April 2022 na unatarajiwa kukamilika tarehe 30 Januari 2023 na itatumia fedha Kiasi cha bilioni 3.
Katika awamu hi ya kwanza vinajengwa vyumba vya madarasa 12, jengo la utawala 1, maabara 4, matundu ya vyoo 16, chumba cha jenereta 1, bwalo 1, mabweni 5, mitaro ya majl, kichomea taka 1, matanki ya chini ya maji, matanki ya plastiki, uzio, njia za kutembea na nyumba za walimu 2.