Katika kuhakikisha serikali pamoja na asasi zisizo za kiserikali zinafanya juhudi za upatikanaji wa nishati mbadala na isiyo haribu mazingira kampuni ya Viridium Tanzania Ltd ambayo inazalisha nishati ya mkaa mweupe kwa kutumia majani ya Tembo ambapo Naibu waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Khamis Hamza Khamis amesema bado kuna haja ya elimu kuzidi kutolewa kwa wananchi ili kuondokana na ukataji wa miti unaopelekea utunzaji wa mazingira .
Naibu waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira ameyasema hayo wakati alipotembelea kiwanda hicho kilichopo kata ya Nzihi na amesema ni vyema sasa wanannchi waache matumizi ya kutumia mkaa , kuni na badala kutumia nishati mbadala kama mkaa mweupe ambapo pia itakuwa rafiki kwa mazingira
“ Niwaombe waendelee kuwekeza nguvu kubwa kuzidi kutoa taaluma kwa wanannchi ya namna bora ya kutumia nishati mbadala kwasababu akili za baadhi ya wanannchi bado ziko kwenye matumizi ya kuni na mkaa kwahiyo kazi kubwa ni kuwabadilisha kutoka kwenye kuni na mkaa na kuwapeleka kwenye matumizi ya mkaa mweupe ili kunusuru afya zao pamoja na kunusuru mazingira “
AYO TV imezungumza na George Fereira ambaye ni Mkurugenzi mkuu wa kiwanda hicho amesema mradi huo umegaribu zaidi ya bilioni 12 kwaajili ya uzalishaji wa nishati ya mkaa mweupe na kiwanda hicho kimetoa ajira rasmi zaidi ya 100 na ajira zisizo za rasmi (vibarua ) zaidi ya 500 kutoka katika maeneo mbalimbali mkoani iringa