Wizara ya Nishati Nchini kupitia Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) limeendelea na Majaribio kwa njia ya maji ya mtambo namba 9 katika mradi wa kufua umeme wa bwawa la Julius Nyerere lililopo Rufiji Mkoani Pwani.
TANESCO wamesema mpaka sasa majaribio hayo yamefanikiwa tayari na kinachosubiriwa ni uwashwaji wa mtambo ili kuanza uzalishaji huo wa umeme, kwenye taarifa yao TANESCO wamesema Wananchi wakae tayari hivi karibuni wanawasha.