Adam Jamal,Samweli Ayo na Laiko ngweta ni miongoni mwa majeruhi wa ajali ya gari Aina ya Kamaz Lori iliyotokea usiku wa kuamkia Novemba 3 mwaka 2024 mkoani Tabora wamehamishiwa Katka hospital ya rufaa ya kanda ya KCMC Moshi baada ya hali zao kuwa mbaya taarifa ya kuhamishwa kwa majeruhi hao Imetolewa na Kaimu Mganga mfawidhi hospitali ya Rufaa mkoa wa Tabora Dkt. Swaumu Kimaro alipokuwa anawasilisha taarifa ya hali ya majeruhi waliopo katika hospitali hiyo ambapo majeruhi hao wamesafirshwa kwa Ndege asubuh ya leo Kuelekea Moshi mkoani kilimanjaro huku idadi ya majeruhi wengine wakitajwa kuongezea.
“Tulipokea majeruhi 30 pamoja na vifo vya watu wawili na katika majeruhi 30 tuliopokea walikuwa wamepata majeraha sehemu mbalimbali za miili yao, na tumeshawaruhusu majeruhi 15 wakiwemo watatu ambao walipewa rufaa kwenda hospitali ya rufaa ya mkoa wa Kilimanjaro KCMC na wengine 12 waliruhusiwa kwakua hawakuwa wameumia na kupata majeraha makubwa na Mpaka sasa tumebaki na majeruhi 15 ambao tunaendelea kuwahudumia kwa wanavyoonekana wanaendelea vizuri na muda wowote wanaweza kuruhusiwa kwaajili ya kwenda nyumbani na ile miili miwili ya waliofariki wameshasafirishwa kuelekea Moshi Kilimanjaro kwa kupewa ndugu zao” Swaumu Kimaro
Mkuu wa mkoa wa Tabora Paul Chacha amewapongeza madaktari wa hospitali hiyo kwa huduma hiyo waliyoitoa kwa majeruhi wanaoendelea kupata huduma. amefika katika hospital ya Rufaa mkoani hapo kutoa pole kwa majeruhi ambao wanaendelea na matibabu huku akiwapongeza madaktari wa hospital hiyo kwa huduma nzuri kwa Wanafunzi hao.
“Tunaendelea kuwashukuru madaktari wa kitete wamefanya kazi kubwa ya kuokoa maisha ya hawa vijana ambao walikuwa wanaenda mafunzo kwa vitendo japo wamefariki wawili lakini hawa waliobahatika kufika hospitali madaktari wamefanya juhudi kubwa na wanaendelea vizuri na wameokoa kwa asilimia 90 mpaka Sasa lakini pia tulikuwa tunafikiri labda kulikuwa na uzembe wowote wa madereva lakini ni msafara ulikuwa na magari saba Ila gari ya kwanza ndio ilikuwa imepata ajali kutokana na tairi kupata pancha kwahiyo hatuna cha kulaumu.”Paul Chacha