Shughuli mbalimbali za kibinadamu zinazofanyika kwenye milima na vyanzo vya Maji vimepeleka athari kubwa kwa wananchi wa jiji la Tanga hususa ni juu ya swala zima la ukosefu wa maji na maji kuwa machafu na hivyo kuhatarisha afya ya watumiaji.
Kutokana na hali hiyo waziri wa maji jumaa aweso alifanya ziara jijini Tanga juu ya kuangali hali ya upatikanaji wa huduma za maji na athari za kilimo zinazofanywa pembezo mwa mito inayo leta maji yake kwenye mto zigi na kuifadhiwa kwenye bwawa la mabayani jijini tanga na kumwagiza mkurugenzi wa bonde la mto pangani kufanya ziara maalumu kutembelea mito iliyo athirika na hali hiyo.
Kutekeleza agizo hilo mkurugenzi wa bonde la Mto pangani Mwandisi Segule Segule amefanya ziara na kutembelea mito hiyo iliyoko wilayani muheza ambapo alisema kuwa bado shuhuli mbalimbali za kibinadamu zinaendelea kama kilimo,uchimbaji wa madini na ujenzi wa madaraja makubwa yanayo jengwa kwenye mito yetu na hivyo kupelekea udongo mwingi kuingia kwenye mito na kusisitiza kuwa kama mamlaka itachukua hatua stahiki kwa wananchi watakao bainika kufanya jambo hilo.‘‘Mto muzi ni mmoja wa mto unaingiza maji kwenye mtozigi tope katika mto huu lipo kwa kiasi kikubwa hii yote inatokana na shuhuli mbalimbali za kibinadamu na ndio inayochangia changamoto kubwa ya tope kwenye mtozigi’’- Alisema Segule Segule
Kwa Upande wa Steven Ndaondi ambaye ni mwenyekiti wa kijiji cha kambani amesema kuwa Uchafunzi wa maji kwenye mto zigi husababishwa na sababu mbalimbali hususa ni mvua za masika ambazo zinaendelea kwenye milima ya amani pamoja na shuhuli za kibinadamu kama kilimo ambapo mvua zinapo nyesha husababisha mmomonyoko wa aridhi na hivyo tope jingi huingia kwenye mito.