Headlines za tukio la kupatwa kwa jua September 1 2016 katika Wilaya ya Mbarali Mkoani Mbeya ni moja ya zile zilizotawala katika mitandao ya kijamii na vyombo mbalimbali vya habari nchini ambapo Serikali pamoja na wananchi wa kawaida walijitokeza kushuhudia tukio hilo.
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makala ni miongoni mwa washiriki waliopata nafasi ya kuhojiwa na Ayo TV ambapo yeye alitazama tukio hili katika upande wa fursa…>>>’Hili ni tukio la kihistoria ambalo limetuwesaidia kujifunza zaidi kwakuwa hata mimi nilikuwa najua kupatwa kwa jua ni mwisho wa dunia‘
‘Lakini kumekuwa na fursa za kiuchumi kama madereva wamefanya biashara nzuri kwa kuwasafirisha watu, mama ntilie wameuza vyakula na wafanyabiashara wameuza matunda na kutangaza mchele wao‘ –Amos Makala
‘Kubwa pia ni kwamba tumetangaza vivutio vya mkoa wetu na sasa tujielekeze katika uchumi wa kuwahudumia watu wetu ili tuweze kuendesha nchi ya viwanda, nasema siasa ni uchumi ambao tunatakiwa tuitumie ili kuwainua wananchi wetu‘ –Amos Makala
Unaweza kuendelea kumsikiliza RC Makala kwenye hii video hapa chini…
ULIMIS TUKIO LA KUPATWA KWA JUA MBARALI MBEYA?