Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Amos Makalla amemuagiza Mkuu wa Wilaya ya Temeke Jokate Mwegelo kuwaelekeza Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA) na wamiliki wa vyombo vya usafiri kuhakikisha ndani ya wiki daladala zinafika kwenye Soko la Kijichi ili kuchagiza biashara sokoni hapo.
RC Makalla ametoa maagizo hayo wakati wa ziara yake ya ukaguzi wa Masoko Wilaya ya Temeke ambapo amesema changamoto za masoko lazima zipatiwe majibu hususani suala la daladala kutokupita katika maeno ya masoko.
“Nimekuja na Mkuu wa Wilaya yeye ndio Mwenyekiti wa Ulinzi na Usalama, LATRA wapo tunataka mabasi yaje hapa DC Simamia, LATRA waite na mimi naagiza ndani ya wiki moja nitakuja nataka kukuta daladala hapa, tusibembelezane dalala zije hapa shida nini watu wakishuka hapa watanunua kitu cha kwanza, watatamani na kitu kingine,” RC Makalla.
Pia RC Makalla ameeleza kuwa baadhi ya watendaji ndio wanakwamisha masoko kutokana na kutokuzipatia ufumbuzi changamoto zilizopo masokoni, huku akisema kuwa baadhi ya ubunifu kwenye masoko hauzingatii utamaduni wakitanzania.
DIAMOND PLATNUMZ, BURNA BOY WALIVYOINGIA KWENYE TUZO ZA BET