Makamu wa kwanza wa rais wa Iran, Mohammad Mokhber, anatarajiwa kuchukua wadhifa wa urais kufuatia kifo cha rais Ebrahim Raisi katika ajali ya helikopta kabla ya kufanyika kwa uchaguzi.
Kwa mujibu wa katiba ya Iran, makamu wa kwanza wa rais anastahili kuchukua wadhifa huo iwapo rais atafariki, kuondolewa madarakani, kujiuzulu au kuwa mgonjwa kwa kpindi cha zaidi ya miezi miwili.
Raisi, ambaye alifariki katika ajali hiyo ya helikopta siku ya Jumapili pamoja na waziri wake wa mambo ya kigeni Hossein Amir-Abdollahian na maofisa wengine wa serikali, alikuwa anakaribia mwisho wa muhula wake wa kwanza wa kipindi cha miaka minne kama rais