Makamu wa Rais wa Tanzania Dkt.Philip Isdor Mpango amezitaka Taasisi za kifedha hasa mabenki kusogeza matawi katika maeneo ya Vijijini ambayo wananchi wamekuwa wakisafiri umbali mrefu kufuata huduma hiyo na wengine kulazimika kutunza fedha majumba ambapo usalama umekuwa mdogo.
Dkt.Mpango ametoa agizo hilo wakati akifungua Tawi la Benki ya Taifa ya baishara NMB katika wilaya ya Buhigwe mkoani Kigoma na kufikia tawi la sita mkoani humo na la 229 nchini nzima.
Katika wilaya ya Buhigwe Mkoani Kigoma baadhi ya wananchi kutoka katika vijiji kadhaa walilazimika kutembea karibu kilometa 140 kwenda na kurudi katika wilaya ya Kasulu kufuata huduma za kifedha katika mabenki kila walipo hitaji.
Tawi la Benki ya NMB linakuwa la kwanza katika wilaya hii ya Buhigwe ambayo sasa imefunguliwa na kutarajiwa kuanza kutoa mikopo ya takribani shilingi bilioni moja kwa wajasiriamlinna wafanyabiashara.
Uzinduzi wa Tawi la benki ya NMB Wilayani Buhigwe umeenda sambamba na utoaji wa misaada ya vitanda kwajili ya shule,Vitanda vya akina mama kujifungulia pamoja na mabati vifaa vilivyo na thamani ya shilingi milioni 82.4.