Makamu wa rais nchini Zimbabwe amesema serikali itazuia ufadhili wa masomo wa chuo kikuu kwa vijana wanaojihusisha na maingiliano ya kingono ya watu wenye jinsia moja (LGBTQ+).
Ufadhili wa masomo ya vyuo vikuu vya serikali kwa watu wa kati ya umri wa miaka 18 na 35 unafadhiliwa na GALZ, shirika la wanachama la LGBTQ+ nchini Zimbabwe. Jumuiya hiyo ilianza kutoa ufadhili huo mnamo 2018.
Makamu wa Rais wa Zimbabwe, Constantino Chiwenga amesema akijibu tangazo la majuzi la jumuiya hilo la kutoa ufadhili kwa watu wanaojihusisha na maingiliano ya kingoni ya jinsia moja kwamba, ufadhili huo ni “changamoto ya moja kwa moja” kwa mamlaka ya serikali.
Constantino Chiwenga amesema: “Shule zetu na taasisi za elimu ya juu hazitawakubali waombaji, achilia mbali kuandikisha majini ya watu wanaohusishwa na maadili ngeni, yanayopinga maisha, yasiyo ya Kiafrika na yasiyo ya Kikristo ambayo yanakuzwa, kuenezwa na kutekelezwa katika jamii zilizooza ambao hatuna uhusiano wowote wa kimaadili au kitamaduni nazo.”
Chiwenga amesema, sheria za Zimbabwe dhidi ya mashoga zinafanya “ufadhili wa masomo yanayoegemezwa juu ya upotovu kuwa kinyume cha sheria na uhalifu, na dharau kubwa na mbaya kwa maadili ya kitaifa.”