Wanajeshi wa Urusi wameshambulia kwa makombora mpaka wa Sumy uliopa ndani ya Ukraine mara 89 siku ya Jumapili, utawala wa kijeshi wa eneo hilo uliripoti.
“Wakati wa mchana, Warusi walifanya mashambulizi 89 kwenye maeneo ya mpaka na makazi katika eneo la Sumy. Milipuko 222 ilirekodiwa.
Mshambulizi hayo yalifanyika katika maeneo ya makazi ya Yunakovskaya, Belopolskaya, Vorozhbyanskaya, Lebedinskaya, Krasnopolskaya, Velikopisarevskaya, Putivlskaya, Novoslobodskaya, Glukhovskaya, Esmanskaya, Shalyginskaya, Druzhbovskaya, Seredino-Budskaya zilichomwa moto,” ujumbe huo unasema.
Kulingana na mamlaka, katika makazi ya Belopol, ambako mabomu ya angani yamerushwa, mtu mmoja aliuawa na watatu walijeruhiwa, akiwemo mtoto wa miaka 11.
Mkazi mmoja wa wa eneo la Yunakovskaya aliripotiwa kujeruhiwa kufuatia mashambulizi hayo, kulingana na mamlaka ya eneo.
Maeneo mengine ya eneo hilo yalipigwa kwa mabomu ya angani, ndege zisizo na rubani za FPV, mizinga na makombora, utawala uliongeza.