Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Paul Makonda leo amenisogezea stori nyingine na kikubwa anachokigusia ni kuhusu kuzindua huduma kwa wananchi ambazo zitawasaidia kwenye maeneo mbalimbali, najua ni wengi wanakutana na matatizo kwenye ofisi za umma ikiwemo Polisi, Hospitali na kwingineko…
Majibu ya nini kitafanyika yako hapa >>> “Kutokana na kero nyingi zinazoendelea na kusababisha watu kukosa huduma, watu wanapiga simu polisi wakiomba msaada kutokana na kuvamiwa, wanaambiwa waweke mafuta kitu ambacho si kazi yake, mtu anakwenda hospitali anakaa siku mbili au tatu hamuoni nesi, ardhi mtu anafatilia kibali cha kujenga zaidi ya miaka mitatu hapati, sisi hatuoni kama kuna sababu ya haya kuendelea kufanyika“
Sentensi za Paul Makonda zinaendelea hivi >>> “Tunaanzisha mfumo utakaowasaidia wananchi kupata misaada kutoka Serikalini , mfano umekwenda hospitali hupati msaada, unachotakiwa kufanya ni kutoa taarifa kwa kuandika ujumbe mfupi kwenda namba 15404 na baadaye utapata ujumbe kutoka kwa ofisi ya Mkuu wa Wilaya na utafanyiwa kazi na wahusika kushtakiwa“.
DC Paul Makonda amesema kingine ni kwamba utaratibu unaoanzishwa sasahivi Wakurugenzi wa kata watapewa taarifa kuhusu malalamiko ya kila eneo husika na kuwaonyesha malalamiko yanayotolewa na wananchi wa maeneo yao.
Ujumbe wote kutoka kwa DC Paul Makonda utausikia ukibpnyeza play hapa…
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE kwa kubonyeza hapa >>>INSTAGRAM, TWITTER, FB, YOUTUBE