Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Paul Makonda leo amekutana na viongozi wa masoko mbalimbali na kuzungumzia kero zinazokabili masoko hayo.
“Nimeitisha kikao cha viongozi wa masoko, wamekuja wote na kujadili afya, vyoo vinayotumika ndani ya masoko, biashara katika ukusanyaji wa masoko, nimeelekeza Afisa bishara na viongozi wa Wilaya ni kuziangalia changamoto hizo ikiwemo kupima eneo la masoko ili yasichukuliwe na wengine”…Paul Makonda
“Asilimia zaidi ya 70 ya masoko yana matatizo mengi, changamoto ya vyoo na hata mipaka ya masoko yao ambayo yanapelekea kufanya kazi katika mazingira magumu na hatarishi kwa afya za Watanzania”…Paul Makonda
Kingine kilichosikika ni kuhusu uvamizi wa maeneo ambayo si rasmi…”Nachoomba wananchi wasilazimishe Serikali ikatumia nguvu, sehemu ambayo unajua kabisa ni hatari kwako na kwa kizazi chako tusilazimishe, kuna baadhi ya watu wamepewa maeneo wakaamua kuuza, naomba kippindi hiki cha mvua watu wachukue tahadhari, wale waliojenga kwenye mito ninawaomba waondoe vifaa vyao mapema, hakuna muda wa kuwasuburi, tayari walishapewa taarifa“…Paul Makonda.
Kuhusiana na mgogoro wa wafanyakazi wa kiwanda cha nguo cha tooku..“Nimefika na kukuta matatizo makubwa ya changamoto ya malipo, matibabu, na mikataba yao ikiwa kwenye mgogoro, nikaelekeza viongozi waliangalie hilo kwa makini ili wafanyakazi waweze kurudi baada ya kugoma, niliwaahidi kumpeleka Waziri wa viwanda na biashara pamoja na Waziri wa kazi na leo walikwenda kiwandani hapo kuangalia hali halisi.
“Waziri alizungumza na uongozi kisha wametoa maelekezo na wameacha timu ya wataalam wakiangalia mikataba na vigezo kuhakikisha wafanyakazi wanalipwa na kuendelea na kazi zao kama kawaida bila kuathiri kiwanda pamoja na wafanyakazi wenyewe”…Paul Makonda.
Sauti ya Paul Makonda..
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyezahapa>>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.