Headlines zenye stori za Siasa zimeendelea kutawala.. Makongoro Nyerere ni Mbunge anaewakilisha TZ kwenye Bunge la Afrika Mashariki, nae alikuwa nyumbani kwao Butiama, hapa nimenukuu sehemu ya kile aichokisema akiwa huko.
“Nina nia ya kutangaza nia lakini bado sijatangaza nia… kwanza tuzungumze kuhusu utaratibu wa CCM. Mkutano Mkuu utakaa tarehe 11 na 12 June ili kuisikia Rasimu ya Chama, kuithibitsha na kuipitisha… Sizuki na kuanza kuzungumza kabla ya ilani ya Uchaguzi.. Wanaoamua nani awe kiongozi sio huku kwenye Chama, ni Watanzania…“>>> Makongoro Nyerere.
Kwenye sentensi nyingine akasema hivi kuhusu wale wanaomzungumzia >>> “Huyo mtoto wa Nyerere huyo ni mlevi kweli… mmewashtukia au vipi??.. Huyo mtoto wa Nyerere huyo anapenda wanawake kweli.. sasa mlitaka nipende wanaume? Nawapenda kweli na mimi nashukuru MUNGU mnanipenda kweli”>>> Makongoro Nyerere.
Makongoro Nyerere akamalizia hivi >>>“CCM sio chama cha vibaka, ni chama cha walio wengi.. wakulima na wafanyakazi.. turudishieni chama chetu, mnaenda nacho wapi? Kufanya nacho nini? Alafu sisi mtuache wapi?”>>>
Utamsikiliza kwa urefu zaidi kila alichokisema kwenye sauti hii mtu wangu
Unahitaji chochote ninachokipata kisikupite? jiunge na mimi kwenye Twitter, Facebook na Instagram kwa kubonyeza hapa >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.