Makumi ya watu wamekufa na wengine kadhaa wameripotiwa kutoweka baada ya boti mbili kugongana kwenye mto Kongo karibu na Kinshasa katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo siku ya Jumatatu.
Katika picha za kushangaza zilizochukuliwa muda mfupi baada ya kugongana, wakaazi waliojawa na hofu wanaweza kuonekana wakitazama kutoka ukingo wa mto huku boti ndogo zikitoka mbio katika harakati za kuokoa abiria.
Haijafahamika mara moja ni wangapi waliokolewa au ni nini kilisababisha ajali kati ya boti hizo mbili zilizokuwa zimesheheni watu na mizigo.
Mito ni muhimu kwa usafiri katika nchi hiyo kubwa ya Afrika ya kati ambayo ina miundombinu duni ya barabara.
Ajali mbaya za boti hutokea mara kwa mara kwani wafanyakazi mara nyingi hupakia vyombo.
Usafiri mwingi wa mtoni unaendeshwa na waendeshaji wadogo wasio rasmi, na maafisa wameonya kuwa uzingatiaji wa kanuni za baharini ni duni.