Rais John Magufuli ametoa siku saba kwa Waziri wa Afya, Dkt. Dorothy Gwajima na Waziri wa TAMISEMI, Seleman Jaffo, wampe majibu ya kwa nini Mkoa wa Geita wanapunjwa Dawa
Akizindua Vituo vya Afya vya Masumbwe na Mbogwe Mkoani Geita amesema, mwaka 2015 bajeti ya Dawa kwa Mkoa huo ilikuwa Tsh. bilioni 2.35 mwaka 2020 ilikuwa Tsh. bilioni 2.75. Bajeti imeongezeka lakini Dawa ni kidogo.