JAMII ya kiislamu nchini imetakiwa kuwahimiza watoto wao kusoma na kuhifadhi kitabu kitukufu cha Qur’an kwani kwa kufanya hivyo kutawarahisishia kufanya vyema katika masomo yao ya kawaida shuleni.
Kauli huyo imetolewa na mkuu wa mkoa wa Morogoro bi Fatma Mwasa katika mashindano ya kusoma na kuhifadhi kitabu kitukufu cha Qur’an mkoani humo mashindano yaliyo andaliwa na umoja wa walimu wa madrasa mkoa wa Morogoro (UWAMAMO).
Aidha Mkuu hiyo wa mkoa ameongeza ni vyema kuwahimiza watoto kushikamana na matendo mema ikiwemo kusoma kwa bidii kitabu kitukufu cha Qur’an kwani kupitia kitabu hicho kitawapa muongozo sahihi katika maisha yao ya hapa Duniani na baada ya kufa kwao
Akisoma risala mbele ya mgeni rasmi makamu mwenyekiti wa (uwamamo) mkoa wa Morogoro Sheikh Kombo Hussein akaeleza mafanikio yao toka kuanzishwa kwa mashindano hayo sambamba na kubainisha changamoto wanazokabiliana nazo ikiwemo vifaa vya kuchapisha
Mashindano hayo ya Qur’an yaliyoandaliwa na umoja wa walimu wa madarsa mkoa wa Morogoro yaliwashirikisha washiriki wa waliyo hifadhi juzuu moja, tano ,ishirini pamoja na juzuu thelathini.
Zawadi mbalimbali zilitolewa huku mshindi wa kwanza wa juzuu thelathini akikabidhiwa zawadi ya pikipiki washindi wengine wakikabidhiwa biaskeli na vyerehani.