Kila siku asubuhi huwa nazisogeza headlines zilizobebwa kwenye kurasa za Magazeti ya Tanzania, Uchambuzi wa stori zote napandisha kwenye account yangu ya Twitter >>>@millardayo. Tayari nimezikusanya na waweza kuzipitia hapa chini moja baada ya nyingine.
Moja ya yalioandikwa ni huu utafiti kwenye gazeti la Mwananchi yenye kichwa ‘Maziwa ya mende yana protini kuliko ya ng’ombe’
#MWANANCHI Mende aina ya Diploptera punctate wameonekana kutoa utomvu kama maziwa yenye protini kuliko ya ng'ombe pic.twitter.com/5hbJ0Zp8Ho
— millardayo (@millardayo) July 28, 2016
Uchunguzi wa wanasayansi umebaini maziwa ya mende yana virutubisho ya protini mara nne zaidi ya ng’ombe. Taarifa ya timu hiyo ya kimataifa ya wanasayansi hao ya ‘Institute of Stem Cell Biology and Regenerative Medicine’ ilisema maziwa hayo yanaweza kuwa muhimu kuwalisha watu wanaoongezeka duniani siku za usoni.
Sehemu ya taarifa hiyo ambayo imenukuliwa na mashirika mbalimbali duniani imesema……>>>’Ingawa mende wengi hawatoi maziwa, mende aina ya Diploptera punctute, wameonekana kutoa utomvu unaoonekana kama maziwa yenye protini yanayotumika kuwalisha watoto’
Taarifa hiyo imesema wadudu nao hutoa maziwa lakini kilichowashangaza zaidi watafiti ni yana nguvu mara tatu zaidi yanayopatikana kwenye maziwa ya kifaru.
#MWANANCHI CHADEMA wabadili gia, watangaza operesheni ukuta na kutangaza mikutano nchi nzima september Mosi pic.twitter.com/IQOC4a1BGf
— millardayo (@millardayo) July 28, 2016
#MWANANCHI Safari ya Tizeba Dom yaingia doa umoja wa mawakala wa pembejeo za kilimo wamtaka awalipe fedha zao kwanza pic.twitter.com/quZmH7NhdS
— millardayo (@millardayo) July 28, 2016
#MWANANCHI Jeshi la polisi K'njaro linawashikilia askari wake 10 ni baada ya mahabusu saba kutoroka pic.twitter.com/xMw5L4zbNS
— millardayo (@millardayo) July 28, 2016
#MWANANCHI TTCL yarudi serikalini kwa 100% baada ya kuilipia Bhart Airtel bil 14.9 iliyokuwa imeingia nayo ubia pic.twitter.com/tKmStvAv95
— millardayo (@millardayo) July 28, 2016
#MWANANCHI Agizo la JPM kuhamia Dodoma laongeza maombi ya viwanja kwa ajili ya majengo ya ofisi pic.twitter.com/HtOgt6o8TJ
— millardayo (@millardayo) July 28, 2016
#NIPASHE Wadaiwa mikopo elimu ya juu wasiojisalimisha kuwekewa vikwazo vya kusafiri nje na kukopeshwa pic.twitter.com/DvUw8SpPj6
— millardayo (@millardayo) July 28, 2016
#NIPASHE Bei za viwanja imepanda maradufu ndani ya siku tano Dodoma tangu kutolewa kwa agizo la kuhamia Dom pic.twitter.com/crbvx9ofAd
— millardayo (@millardayo) July 28, 2016
#NIPASHE Serikali imetoa mwezi mmoja kwa wanaoghushi nembo za Taifa ikiwamo 'bendera na ngao' kuacha mara moja pic.twitter.com/aDtZu4PXCD
— millardayo (@millardayo) July 28, 2016
#MAJIRA DC Gondwe apiga marufuku waganga wa tiba za jadi wanaopita kwenye nyumba na kudai wanafichua wachawi Handeni pic.twitter.com/GyV8xtOgKl
— millardayo (@millardayo) July 28, 2016
#JamboLEO NEC imesema mchakato wa katiba mpya utafufuka baada ya kukamilika kwa maboresho ya sheria ya kura ya maoni pic.twitter.com/X0a6pB6DwT
— millardayo (@millardayo) July 28, 2016
#HabariLEO Ripoti ya 2016 ya uchumi wa simu za mikononi Afrika imesema TZ ni miongoni mwa nchi nane zenye soko kubwa pic.twitter.com/Y0fbqerUnO
— millardayo (@millardayo) July 28, 2016
#MWANANCHI Mgodi wa dhahabu Nyamahuna wafungwa kupisha uchunguzi wa kifo cha Elisha, inadaiwa alianguka kwenye ngazi pic.twitter.com/rkfQ0VAAop
— millardayo (@millardayo) July 28, 2016
ULIKOSA UCHAMBUZI WA MAGAZETI JULY 28 2016 KUTOKA AYO TV? UNAWEZA KUANGALIA VIDEO HII HAPA CHINI