January 28 Rais wa shirikisho la mpira wa miguu Tanzania TFF Jamal Malinzi alifanya mkutano na waandishi wa habari makao makuu ya shirikisho hilo na kutangaza msiba wa aliyekuwa mjumbe wa kamati ya utendaji ya TFF na Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu mkoa wa Simiyu Epaphra Swai.
Malinzi pia ametumia fursa hiyo kuomba radhi vilabu 15 vya Ligi Kuu kufuatia lile sakata linalopingwa na Simba la kuwapa ruhusa Azam FC kucheza mechi za kirafiki na kuahirishiwa baadhi ya michezo yao ya Ligi, kitu ambacho Simba wanahofu ya kuwa kuahirishwa kwa mechi hizo kunaweza kutengeneza mazingira ya kupanga matokeo.
“Kiukweli naomba nivitake radhi vilabu vyote 15 vya Ligi kwa kosa lililofanyika la kuwaruhusu Azam FC kwenda Zambia kucheza mechi za kirafiki, najua maamuzi yamefanyika mimi nikiwa Burundi, lakini kama kiongozi nakiri kosa kufanyika na naviomba radhi vilabu vyote, kuhusu Yanga kutofanya uchaguzi ukweli ni kuwa Yanga hawapo juu ya sheria na wanapaswa kuheshimu katiba yao na ya TFF” >>> Jamal Malinzi
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyezahapa>>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.