August 20 Rais wa shirikisho la mpira wa miguu Tanzania TFF Jamal Malinzi alithibitisha kukubaliwa na mmiliki wa klabu ya Orlando Pirates ya Afrika Kusini Irvin Khoza kupeleka vijana watano wenye umri wa miaka 15 kwenda kufanyiwa majaribibio katika klabu hiyo na kama watafuzu watachukuliwa.
Malinzi amehakisha kuendelea na mipango ya kusambaza wachezaji vijana katika nchi mbalimbali duniani ili waweze kukuzwa katika mazingira ya soka hivyo anaongea na vilabu vingine vya nchi ya Ureno ili kuweza kupeleka wachezaji wengine katika nchi hiyo.
“Namshukuru Irvin Khoza mmiliki wa Orlando Pirates nimemuomba na amekubali Tanzania tumpelekee vijana wa tano wazuri kutoka katika under 15 tuliyonayo sasa hivi, Orlando Pirates watawachukua na watawafanyia majaribio wakiona wanafaa wataingia katika Academy yao”>>> Jamal Malinzi
Hii ni sauti ya Malinzi akithibitisha mpango huo.
PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia za siasa muziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos