Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu @heslb_tanzania imewakumbusha Wanafunzi wanufaika wa mikopo ya elimu ya juu kuwa malipo ya fedha za mikopo inayotolewa na Serikali kupitia HESLB yanalipwa na kupokelewa na Mwanafunzi-mnufaika kupitia akaunti yake ya benki aliyoichagua na kuisajili kupokelea fedha za mkopo wake.
Ufafanuzi huu umetolewa kufuatia maswali na maoni kutoka kwa Wadau mbalimbali wakiwemo Wanafunzi wanufaika wa mikopo pamoja na Viongozi wa Serikali za Wanafunzi.
Itakumbukwa kuwa kupitia matangazo ya Bodi hiyo kwa Waombaji mkopo wa mwaka 2023/2024 yaliyotolewa kuanzia July hadi October, 2023, iliwasihi Wanafunzi wote Waombaji wa mkopo na wanufaika kufungua akaunti za benki katika Taasisi za fedha za chaguo lao.
“Hivyo, ufafanuzi huu unalenga kuwakumbusha Wanafunzi-Wanafuika wa mikopo kuwa taratibu na mifumo ya malipo ya fedha za mikopo ya HESLB inaruhusu Wanufaika wote kulipwa kwa wakati kupitia akaunti za benki mbalimbali walizozichagua, kila mnufaika aliyekamilisha taratibu za usajili chuoni na kwenye mfumo wa malipo wa HESLB (DiDiS) atalipwa fedha zake kwa wakati kupitia akaunti ya benki aliyoichagua”