Malori mengine 20 ya misaada yanatazamiwa kuwasili Gaza leo, afisa mkuu wa Umoja wa Mataifa amesema.
Vifaa hivyo vitaingia katika eneo hilo kutoka Misri, afisa huyo aliongeza.
Siku ya Jumamosi, malori 20 yaliingia Gaza katika shehena ya huduma ya kwanza katika eneo hilo tangu Israel ilipoweka mzingiro kamili mwanzoni mwa vita.
Israel kisha ikaruhusu msafara wa pili wa lori 15 kuingia Gaza siku ya Jumapili.
Msafara wa tatu mdogo wa misaada kutoka Misri uliingia Gaza siku ya Jumatatu.
Waliingia kutoka Misri kupitia kivuko cha Rafah – njia pekee ya kuingia Gaza isiyotawaliwa na Israeli.