Malori sita ya misaada yalivuka kutoka Israel moja kwa moja hadi kaskazini mwa Gaza kama sehemu ya mradi wa majaribio wa kuhakikisha usambazaji wa vifaa katika eneo hilo, jeshi la Israel lilitangaza.
Kulingana na jeshi, malori sita ya misaada ya Mpango wa Chakula Duniani (WFP) “yaliingia kaskazini mwa Ukanda wa Gaza kupitia lango la ’96’ kwenye uzio wa usalama” mwishoni mwa Jumanne.
Jeshi hilo lilisema lilifanyika kama sehemu ya majaribio, na kubaini kuwa lori hizo zilikaguliwa hapo awali Kerem Shalom.
“Matokeo ya majaribio yatawasilishwa kwa maafisa wa serikali.”
Israel imedumisha udhibiti mkali wa misaada inayoingia Gaza tangu kuzuka kwa vita vyake huko Gaza, ikikagua shehena huko Nitzana na Kerem Shalom kabla ya kuziruhusu kuingia kusini mwa eneo hilo.
Mashirika ya misaada yamekuwa yakionya juu ya hatari ya njaa katika Gaza iliyozingirwa kwa wiki kadhaa, na Umoja wa Mataifa umeripoti ugumu fulani katika kufikia eneo la kaskazini mwa eneo hilo kwa ajili ya kupeleka chakula na vifaa vingine vya kibinadamu.