Jeshi la Polisi Mkoani Mbeya, limemrejesha mkoani Mbeya mwanamke mmoja ajulikanaye kwa jina la Atughanile Kalenga, ambaye alikamatwa akiwa jijini DSM kwa amri ya Mkuu wa Mkoa, Albert Chalamila akituhumiwa kutapeli viwanja vya watu na kuviuza.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mbeya, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi, Ulrich Matei amemkabidhi mwanamke huyo kwa Chalamila wakati wa Mkutano wa Hadhara uliofanyika katika Mtaa wa Gombe ili ajibu tuhuma zinazomkabili.
Katika Mkutano huo Chalamila aliliagiza Jeshi la Polisi mkoani humo kuwatafuta watu wengine waliokuwa wanashilikiana na mwanamke huyo kutapeli viwanja akiwemo mme wake na aliyekuwa Ofisa Mtendaji wa Mtaa wa Gombe Kasikazini ambaye kwa sasa alishahamishiwa katika Kata ya Iganzo jijini humo.