Afisa aliyekuwa anafanya kazi ya kukatisha tiketi amefariki baada ya kutemewa mate na mwanaume mmoja anayedaiwa kuwa alikuwa na maambukizi ya virusi vya Covid-19.
Belly Mujinga, 47, ambaye alikuwa na matatizo ya kupumua, alikuwa akifanya kazi katika kituo cha Victoria Jijini London mwezi Machi alipodhalilishwa, sambamba na mfanyakazi mwenzie wa kike.
Ndani ya siku kadhaa baada ya tukio hilo, wanawake wote waliugua ugonjwa wa Covid-19
Polisi wamesema kuwa madai yamefunguliwa ili kumtafuta mwanaume aliowatemea mate wanawake hao wawili. Bi. Mujinga alikuwa kwenye kituo hicho tarehe 22 mwezi Machi wakati alipokabiliwa na mshukiwa huyo.