Jeshi la Polisi Mkoani Shinyanga linamshikiria Mwanamke alifefahamika kwa Jina la Nyansololi Poul Mkazi wa Kijiji cha Kishapu Kata ya Mwantini wilaya na Mkoa wa Shinyanga kwa tuhuma za kumuuwa Mtoto wake Nazael Kidia Mwenye umri wa mwaka mmoja na miezi Saba.
Akizungumza na wandishi wa habari Ofisini kwake Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga SACP Janeth Magomi amesema mtuhumiwa Baada ya kukamatwa na Polisi ahojiwa huku akisema Mtoto wake amemchinja na kumla huku tatizo la Afya ya akili likitajwa na ndugu zake kuwa Miongoni mwa chanzo cha tukio hilo.
“Ni kwamba huyu Mtuhumiwa nyansoli Poul aliishi nyumba moja na mama ake mzazi anaitwa njile kashinje pamoja na wadogo zake mnamo tarehe 4 mwezi wa kwanza 2024 majira ya saa tano za Ahsubuhi aliondoka akiwa na mtoto wake huyo niliyemtaja na akielekea kusiko julikana , ” SACP. Magomi.
” Mtuhumiwa huyo Alirudi nyumbani akiwa hana mtoto wanafamilia walipomhoji kwanini hana mtoto alichokisema ni kwamba kuwa yeye amemla mtoto wake Mkuu wa upelelezi wilaya ya shinyanga alifika kwenye familia hiyo nakuanza uchunguzi wa tukio hilo mara moja pia katika mahojiano na Askari polisi wapelelezi mtuhumiwa alisema kwamba alimuuwa na kumla nyama mtoto huyo, ” SACP.Magomi.