Baada ya Polisi Mkoani Kilimanjaro kutoa taarifa za Kijana mmoja kuuawa na Mtoto wa miaka 12 kwa madai ya kuwa na uhusiano wa kimapenzi na Mama yake, Mama wa Mtoto huyo Mary John amesema ni kweli Mtoto huyo amekiri kuhusika na mauaji lakini hakukusudia kufanya hivyo.
Mary John amesema hakuwa na uhusiano wowote na Kijana aliyeuawa na Mtoto wake bali ni maneno tu ya Watu.
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro James Manyama amesema taarifa walizonazo ni kwamba Mtoto alimkuta kijana huyo chumbani kwa Mama yake ukatokea mzozo na akachukua jiwe na kumpiga kisogoni.
MASHINE ZA NIDA ZAIBIWA ARUSHA,MLINZI ASEMA HAKUONA MLANGO UKIVUNJWA