Ripoti iliyonifikia nikutokea Mkoa wa Geita, Makamu wa rais wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan aliwasili Geita jioni ya leo na akakutana na uongozi wa mkoa wa Geita, Inshu ni wananchi wanufaike na mgodi wao wa dhahabu Geita Geita Gold Mine.…kutana na sentensi zake; Makamu wa rais Mama Samia
‘Wakati nilipopita kwenye kampeni nilipita kwenye mgodi wa Geita Gold Mine nikaangalia hali ya watu wa Geita nikawa na majonzi makubwa…sikuridhika kuwa na mgodi mkubwa kama ule na hali ya watu wa Geita iko ilivyo hivi nikawa sikuridhika nilikuwa mkali kidogo;- Mama Samia Suluhu
‘Wakati naangalia presentation nimeona amount nzuri kidogo inatolewa kwenda kwa watu ingawa bado ninamaswali yangu ambayo nitayafanyia kazi ili tuone ni kiasi gani sahihi kinatakiwa kutolewa na mgodi kwenda kwa wananchi, dhahabu iliyopo niyawana Geita Mungu amewaumbia katika aridhi yao; Mama Samia Suluhu
‘Hatukatai kuwa na wawekezaji wachimbe lakini uchimbaji uwe na faida kote wao wapate na wananchi wapate kwa hiyo hatunabudi kusimamia vizuri na kuhakika kwamba wananchi wa Geita wanafaidika na rasilamali ambayo Mwenyezi Mungu amewapangia;-Mama Samia Suluhu Makamu wa rais
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyezahapa>>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE