“Tanzania na Kenya tulikuwa na vikwazo vya biashara 64 kati yetu, tumeondoa vikwazo 46 hivyo, biashara imekua kutoka bilioni 885 mpaka trilioni 1.1, kwa upande wa uagizaji bidhaa, Kenya iliagiza bidhaa kutoka Tanzania zaidi ya mara tatu ukilinganisha na mwaka 2020 “
“Pamoja na kupunguza vikwazo, tumebaini bado kuna changamoto hivyo, Mawaziri wetu wa Biashara waendelee kukutana na kujadili changamoto zilizobaki ili tuondokane na vikwazo na kukuza biashara”
“Tumekubaliana na zoezi la kuimarisha mpaka ambapo tumeacha kazi kwa Mawaziri wanaohusika na sekta hiyo wakalimalizie, tusaini na tusherehekee kwamba tumeweka mipaka na alama zetu “
“Tumekubaliana kushirikiana katika kupambana na UVIKO – 19, tumewaelekeza Mawaziri wa Afya waende wakashirikiane ili tulifanyie kazi suala hili kwa sababu sote ni wahanga”
“Tumekubaliana kushirikiana katika Sekta ya Utalii, Mawaziri wetu wazungumze waone changamoto gani zipo na zipi ziondolewe ili nchi zote mbili tufaidike kuleta Watalii wengi na kupata mapato mengi zaidi” ——— Rais Samia mbele ya Rais Uhuru Kenyatta leo Ikulu Dar es salaam