Dkt. Hussein Mwinyi tayari amekula kiapo hii leo Novemba 2, 2020, cha kuwa Rais wa awamu ya 8 wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi.
“Nasimama mbele yenu kwa mara ya kwanza nikiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, muda mfupi uliopita nimekula kiapo cha kuwa Rais wa 8, nasimama kwa unyenyekevu mkubwa sana kushukuru” Mwinyi
“Asante Watu wa Zanzibar kwa kura zenu, Serikali nitakayoiunda itaongozwa kwa misingi ya haki, uwajibikaji, uwazi na usawa kwa Wananchi wote bila ya kubagua Mtu yoyote kutokana na itikadi yake, jinsia au eneo analotoka sote ni wa moja” Mwinyi
“Nawapongeza wagombea wenzangu wa Urais ambao wameyakubali matokeo ya uchaguzi na kuyaheshimu maamuzi ya Wananchi, natoa shukrani kwao kwa kuahidi kushirikiana na Serikali nitakayoiunda katika kuwatumikia Wazanzibar” Mwinyi
“Kujitokeza kwenu kwa wingi kupiga kura ni kielelezo cha kukomaa kwenu kisiasa na kidemokrasia na kutambua kuwa uchaguzi ndiyo njia sahihi ya kupata viongozi wa Nchi yetu kwa misingi ya sheria na katiba” Mwinyi
UWEZO WA MAKOMANDO WA JWTZ, UTABAKI MDOMO WAZI