Club ya Sepsi OSK ya Romania imeripotiwa kukubali ofa ya euro 700,000 (Tsh Bilioni 1.9) kutoka Club ya Mamelod Sundowns ya Afrika Kusini ili imuachiea Pavol Safranko (26) ajiunge nao.
Mshambuliaji huyo Pavol ambaye ni raia wa Slovakia amefunga magoli 7 assist 4 katika michezo 25 akiwa na Sepsi OSK huku usajili huo ukitajwa kuwa mkubwa zaidi kuwahi kufanyika katika historia ya Club hiyo ya Ligi Kuu Romania.
Pavol amewahi kucheza timu ya taifa ya Slovakia akicheza jumla ya mechi 10, habari hii inakuwa kubwa Afrika sababu ni nadra sana wachezaji wanaocheza Ligi Kubwa Ulaya au Bara la America kuja Afrika ila Mamelod wameanza kuonesha njia kwa kuwaleta watu kama Gaston Sirino kutokea Uruguay na kuonesha uwezo mkubwa.
Ukiangalia katika viwango vya soka duniani vya FIFA, taifa la Slovakia analotokea Pavol liko nafasi ya 36 kwa ubora huku Romania anakocheza wako nafasi ya 43 kidunia na anakuja Afrika Kusini katika taifa lililo nafasi ya 75 hivyo inatafsirila kama dalili njema kwa soka la Afrika kuleta wachezaji wa viwango.