Vituo vya usajili wa upigaji kura vilifunguliwa mapema leo na ndani ya saa chache watu walionekana kumiminika ili kusajiliwa.Uchaguzi wa mitaa na bunge unatarajiwa kufanyika mwezi wa 12 mwaka huu.
Katika shughuli hiyo ya usajili kuna baadhi ya changamoto zimeshuhudiwa kama vile wengine kukosa kusajiliwa kwasabababu ya uhaba wa karatasi za usajili na hata tarakilishi kutofanya kazi
“Ni ngumu kidogo, kusema ukweli, kwa sababu mambo hayaendi vizuri. Wanasema kwamba karatasi zimekamilika, mashine hazifanyi kazi.
Hakuna ila mabishano. Unaona, haisongi,” Sarath Sidibe, ambaye ni mpishi alisema kutoka kituo kilichoko katika mji mkuu wa Lome.
Katika jaribio lake la pili Komlan Edoh, seremala, alifanikiwa zaidi “Jana nilikuwepo lakini kwa vile watu walikuwa wengi na nina mambo mengine ya kuhangaikia ndiyo maana niliondoka lakini leo nimekuja saa sita imekwenda vizuri nikapokea kadi yangu,” alisema. .
Kama wapiga kura wengi wa 2018 Toganou alikataa kupiga kura baada ya vyama vikuu vya upinzani kuwataka watu kususia uchaguzi wa wabunge.
Mnamo mwaka wa 2018, chama cha Rais Faure Gnassingbé ,kilipata wingi wa viti 59 kati ya 91 vya Bunge la Kitaifa, huku viongozi wa muungano mkuu wa vyama 14 vya upinzani wakisusia uchaguzi.
Waligadhibika baada ya zaidi ya mwaka mmoja wa mgogoro mkubwa wa kisiasa na maandamano kadhaa, ambayo yalikandamizwa vikali, dhidi ya mageuzi yanayomruhusu rais kugombea tena uchaguzi wa 2020 na 2025.
Ni wazi kuwa watu wengi kati ya milioni nane wa Togo wanataka mabadiliko.