Ilikuwa tamasha la ajabu wakati jua lilipotea nyuma ya kivuli cha Mwezi huko Amerika Kaskazini siku ya Jumatatu kutazamwa na makumi ya mamilioni ya watu.
Tukio hili hasa hutokea wakati wa mpangilio wa ulimwengu, Mwezi ulisogea kati ya Dunia na Jua, ukizuia mwanga wake katika kupatwa kamili kwa jua.
Watu walisafiri kwenye sehemu mbalimbali kuvuka Mexico, Marekani, na Kanada ili kutazama kwa mshangao mchana ukigeuka kuwa usiku.
Kwa jumla ilidumu hadi dakika 4 na sekunde 28 katika maeneo fulani,na tukio hili halitaonekana tena nchini Marekani hadi Agosti 2044.
Maafisa wa utalii nchini Marekani wanaamini kati ya watu milioni nne hadi tano walisafiri kutoka sehemu nyingine za nchi kushuhudia maonyesho hayo ya ulimwengu.
Kupatwa kamili kwa jua kutatokea mwaka wa 2026, kukiwa na eneo dogo la Greenland, Iceland, Uhispania, Urusi na eneo dogo la Ureno pekee.
Watu barani Afrika watalazimika kungoja hadi Agosti 2027, wakati kupatwa kamili kutaonekana nchini Uhispania na kaskazini mwa bara hilo.
Kusini mwa Afrika itaona kupatwa kwa jua asubuhi mnamo Novemba 2030 na njia ya jumla kupita Namibia, Botswana, Lesotho, na Afrika Kusini.